Arsenal

Arteta afurahia urejeo wa Jesus

Joel JJ By Joel JJ
14 Mar 2023
Arteta afurahia urejeo wa Jesus

Arsenal hawana muda wa kupumzika kulingana na vile ratiba ya mechi zao ilivyo

Kikosi cha Mikel Arteta kilicheza mechi nyingi katika mwezi uliopita na bado kinaweza kukabiliana na michezo mingine 17 kabla ya mwisho wa msimu

The Gunners wanaweza kutwaa taji la Premia  na kombe la Uropa kwa mara ya ppili

Yatakuwa mafanikio makubwa kwa Arsenal msimu huu, lakini bado kuna mechi nyingi za kucheza

Ushindi wa 3-0 wa Jumapili dhidi ya Fulham ulimaanisha Arsenal kurejea uongozi wao wa pointi tano kileleni mwa Ligi ya Premia.

Kurejea kwa Gabriel Jesus baada ya miezi mitatu nje ya uwanja, kulimpatia Arteta imani mpya

 "Kaongeza nguvu, ni mechi yake ya kwanza leo baada ya muda mrefu. Hatukujua kama ulikuwa mchezo sahihi leo," Arteta alikiri baada ya mchezo.

“Aliniambia siku chache zilizopita 'bado sijawa sawa' lakini jana akaniambia 'nipo tayari' nikasema sawa tukapata fursa ya kumpa nafasi"

"Ni hatua ya kwanza ya kumpa nguvu kubwa. Anaonekana kuwa huru, anaonekana tayari na mara moja alitengeneza nafasi hizo mbili kubwa. Ni vyema kuwa naye tena," alisema Arteta

Mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Europa Alhamisi dhidi ya Sporting CP unatoa fursa nzuri kwa Arteta kutoa dakika zaidi kwa ajili ya Jesus.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishiriki kwa dakika 13 katika Craven Cottage na anaweza kupata dakika nyingi zaidi katika mchezo ujao

Wachezaji watatu ambao walikosa sare ya wiki iliyopita mjini Lisbon wote walirejea uwanjani haraka. Martin Odegaard na Kieran Tierney walikosa mechi ya kwanza kutokana na ugonjwa huku Leandro Trossard akiwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi tatu za mabao katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa ugenini katika historia ya Ligi Kuu

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
13h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
13h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
15h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
16h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
17h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
17h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
17h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
17h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
18h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
19h ago
READ MORE →