Baaada ya kuambulia kipigo cha mabao 1-2 nyumbani kutoka kwa Ruvu Shooting, mashabiki wa Mbeya City wamemjia juu kocha wao, Mubiru Abdallah
Mbeya City wanasuasua kwenye ligi msimu huu hali inayowafanya kuwa kwenye hatari ya kuingia katika janga la kushuka daraja licha ya kushika nafasi ya kumi
Wagonga nyundo hao wa Jiji la Mbeya, wamejikusanyia alama 27 katika michezo 25 waliyocheza, bado michezo mitano kumaliza msimu huu
"Kocha anazingua sana na mbinu zake zimefeli kabisa maana unaona timu haina uwezo kabisa wa kupambana tofauti na msimu uliyopita," alisema mmoja wa mashabiki hao
Mbeya City katika michezo mitano iliyosalia, mitatu itacheza ugenini dhidi ya Namungo FC, Kagera Sugar na Geita Gold



