Mayele alipumzishwa kuwasubiri Monastir - Kamwe

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th March 2023


Mayele alipumzishwa kuwasubiri Monastir - Kamwe

Wakati Yanga ikiibamiza Geita Gold mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Azam Complex, mshambuliaji kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga Fiston Mayele hakuwa sehemu ya mchezo huo

Wengi walihoji kulikoni Mayele ambaye anawania ufungaji bora kwenye ligi kuu msimu huu akiwa na mabao 15, alikosekana hata katika orodha ya wachezaji wa akiba?

Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Mayele alipata majeraha madogo katika mchezo dhidi ya Real Bamako na kwa ushauri wa madaktari wakipendekeza mchezaji huyo asitumike mchezo dhidi ya Geita Gold

"Mayele alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Real Bamako, madaktari walishauri apate muda wa kupumzika ili aweze kupona vyema ndio maana hamkumuona kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold. Tunafurahi anaendelea vyema na sasa anashiriki mazoezi ya timu. Tunaamini mpaka kufika Jumapili siku ya mchezo dhidi ya Monastir atakuwa fit," alisema Kamwe

Yanga inaendelea kujifua Avic Town kujiandaa na mchezo dhidi ya Real Bamako ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu ili kutinga robo fainali michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.