Manchester City

Nimefuata Ligi ya Mabingwa Man City - Haaland

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Mar 2023
Nimefuata Ligi ya Mabingwa Man City - Haaland

Mshambuliaji kinda wa Manchester City Erling Haaland ametamba kuwa alisajiliwa na timu hiyo ili kuwasaidia kushinda Ligi ya Mabingwa kwa sababu tayari wanajua jinsi ya kushinda Ligi ya Premia.

Haaland, 22, jana alifunga mabao matano katika ushindi wa 7-0 wa City dhidi ya RB Leipzig na kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa

Manchester City wanalisaka taji la kwanza mafanikio yao makubwa ikiwa ni kumaliza nafasi ya pili mwaka 2021 wakifungwa kwenye fainali na Chelsea Fc

"Bila shaka klabu inataka kushinda Ligi ya Mabingwa. Wameshinda mataji manne kati ya matano ya mwisho ya Ligi Kuu. Hawakunileta kushinda Ligi Kuu kwa sababu tayari wanajua jinsi ya kushinda"

"Kwa hivyo, unaweza kusoma niko hapa kujaribu kusaidia klabu kujiendeleza zaidi na kushinda Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza," alisema Haaland

Manchester City wameshinda mataji 17 tangu Sheikh Mansour achukue klabu hiyo mwaka 2008, yakiwemo mataji sita ya Ligi Kuu ya Uingereza, manne kati ya hayo yamepatikana baada ya Pep Guardiola kuteuliwa mwaka 2016.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
3h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
10h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’