Real Madrid na Napoli jana zilizungana na timu nyingine sita kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kushinda mechi zao
Mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Real Madrid waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool ukiwa ni ushindi wa jumla wa mabao 6-2 katika mechi zote mbili
Napoli wameendelea kuwatishia vigogo barani Ulaya wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt ukiwa ni ushindi wa jumla wa mabao 5-0
Timu hizo zimeungana na Chelsea Fc, Ac Milan, Inter Milan, Benfica, Manchester City na Bayern Munich katika hatua ya robo fainali
