Klabu ya Manchester City imemuongeza mkataba mshambuliaji Muargentina Julian Alvarez hadi mwaka 2028
Kulingana na Mwanahabari Fabrizio Romano, makubaliano ya mkataba mpya yameafikiwa Alvarez akiridhia kuongeza mwaka mmoja zaidi katika mkataba waka wa awali
Nyota huyo pia atakuwa na ongezeko kubwa la Mshahara baada ya kiwango bora alichoonyesha kwenye michuano ya kombe la Dunia akiisaidia Argentina kushinda taji hilo
"Alvarez amefirahishwa na 'project' ya Manchester City, taarifa zaidi itatolewa na Manchester City wakati wowote," aliandika Fabrizio kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii



