Kuna uwezekano mkubwa Mkufunzi wa Tottenham Hotspurs Antonio Conte ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu pale mkataba wake utakapomalizika
Wiki chache zilizopita Conte alirejea mapumzikoni Italia baada ya kufanyiwa upasuaji
Watu wa karibu na kocha huyo wamedokeza kuwa Conte alifurahia kuungana na familia yake wakibainisha kuwa hafurahii sana kuishi katika hoteli huko London.
Pia Conte hana uhusiano mzuri na Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy, ambaye tayari ameanza mchakato wa kutafuta mbadala wake.
Mauricio Pochettino na Thomas Tuchel wako juu ya orodha ya Spurs na, ingawa hali ya Conte bado inaweza kubadilishwa, kuna uwezekano mkubwa akaondoka.