Simba

Simba kuisaka robo fainali dhidi ya Horoya Ac leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Mar 2023
Simba kuisaka robo fainali dhidi ya Horoya Ac leo

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba leo wanatupa karata muhimu uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo dhidi ya Horoya Ac

Ni mchezo muhimu kwa Simba kuisaka tiketi ya kutinga robo fainali, ushindi wa aina yoyote utawahakikishia Wekundu wa Msimbazi kutinga robo fainali ya tatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita

Hautakuwa mchezo mwepesi kwa kuwa kila timu ina nafasi ya kusonga mbele kama itapata matokeo mazuri

Horoya Ac wanaweza kufurahia alama moja wakifahamu mechi yao ya mwisho wako nyumbani dhidi ya Vipers Fc wakati Simba itasafiri Morocco kuhitimisha hatua ya makundi kwa mchezo dhidi ya wababe Raja Casablanca

Silaha kubwa ya Simba katika mchezo wa leo ni mashabiki wake. Matarajio ni kuwa mashabiki 60,000 watajitokeza kuwaongezea hamasa wachezaji wao

Mkufunzi wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kiko tayari, ari na morali ya wachezaji iko juu na wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo wa leo

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’