Nahodha Taifa Stars Mbwana Samatta anayekipiga KRC genk, winga Simon Msuva anayekipiga Al-Qadsiah FC ya Saudi Arabia pamoja na nyota wengine wanaocheza nje ya nchi walioitwa Taifa Stars wanatarajiwa kuungana na wenzao nchini Misri wakati timu hiyo itakapojiandaa kukabiliana na Uganda
Stars inatarajiwa kuvaana na Uganda kwenye mechi ya Kundi F itakayopigwa Misri Machi 24 kuwania fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika mwakani nchini Ivory Coast

Mbali na Samatta na Msuva, wengine ambao wataunga na Stars ikiwa Misri ni Himid Mao 'Ninja' anayecheza soka la kulipwa nchini humo, Kelvin John na Novatus Dismas (Ubelgiji), Haji Mnoga na Ben Starkie (England) na Ramadhan Makame ambaye anatokea Uturuki
Nyota wengine wa ndani isipokuwa wale wanaoitumikia Yanga, waliondoka nchini mapema leo kuelekea Misri kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kuikabili uganda katika mchezo utakaopigwa huko Misri
Stars inashika nafasi ya tatu kundini nyuma ya vinara Niger yenye pointi mbili na Algeria inayoongoza kundi na pointi sita kila timu ikiwa imecheza mechi mbili, ikusanya pointi moja sawa na Uganda inayoburuza mkia.



