Ni El Clasico; Barcelona vs Real Madrid

Joel JJ By Joel JJ β€’ 19th March 2023


Ni El Clasico; Barcelona vs Real Madrid

Leo Jumapili, March 19, Barcelona na Real Madrid watakutana kwenye mechi ya El Clasico yao ya nne msimu huu.

Barcelona tayari wako mbele kwa pointi tisa kwenye ligi, na kufanya huu kuwa mchezo muhimu kwa Real Madrid kwani kama watafunga watafifisha matumaini ya kutetea ubingwa wao.

Vijana wa Xavi bado wanaweza kushinda ligi kwa kupoteza katika mechi hiyo, lakini ushindi katika dimba lao la Spotify Camp Nou unaweza kukuza faida yao hadi pointi 12

Wakati El Clasico ikiwa mechi kubwa katika La Liga iliyojijengea heshima dunia kote, kashfa ya hivi karibuni iliyoikumba Barcelona imeibua sura mpya kati ya vilabu hivyo.

Mashtaka ya rushwa yamewasilishwa na waendesha mashtaka dhidi ya marais wa zamani wa Barca kutokana na malipo yaliyotolewa kwa kampuni inayomilikiwa na mwamuzi Jose Maria Enriquez Negreira.

Wakati Barcelona ikikanusha makosa yoyote kutokana na malipo hayo, imani ni kwamba malipo hayo yalikuwa kwa Barcelona kupokea upendeleo kutoka kwa waamuzi, jambo ambalo Real Madrid wamewahi kulizungumza

Wakati Real Madrid hawakujumuishwa katika kashfa hiyo, lakini walihusika na Barcelona katika harakati za kuunda Uropa Super Cup, mashtaka yaliyofikishwa mahakamani yameifanya Los Blancos kuanza kujitenga na Barca.

Ingawa inaweza isionekane uwanjani wakati wa mechi ya leo, ni jambo ambalo linaweza kuwa na athari zaidi baadae


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.