Meneja wa Manchester United Erik ten Hag yuko mbioni kuongezewa mkataba wa miaka mitatu, licha ya mazungumzo yanayoendelea kuhusu uwezekano wa kuuzwa kwa klabu hiyo. (Mirror)
Chelsea wanataka kumsajili mlinda mlango wa Leeds United Mfaransa Illan Meslier, 23, katika dirisha kubwa lijalo la usajili. (Football Insider)
Newcastle United wako katika mipango ya kutaka kumnunua winga wa Bayer Leverkusen Mfaransa Moussa Diaby, 23, na beki wa kushoto wa Uholanzi Mitchel Bakker, 22. (90min - in Germain)
Mshambulizi wa Liverpool na Brazil Roberto Firmino, 31, anataka kusalia Ulaya atakapoondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)
Wakala wa Mohamed Salah, Ramy Abbas Issa amepuuzilia mbali uvumi unaosema kuwa Mo Salah anataka kuondoka Liverpool.(90Min)
Liverpool na Manchester United wote wanavutiwa na mlinda mlango wa Anderlecht Mholanzi Bart Verbruggen, 20. (Het Laatste Nieuws )
Liverpool haitampa mkataba mpya kiungo raia wa Guinea Naby Keita, mkataba wake wa sasa utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu huku Inter Milan ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Calciomercato)
Fowadi wa Ghana Mohammed Kudos anamalengo ya kuisaidia Ajax kutetea taji la ligi ya Uholanzi. Kuliko kujali tetesi za kuhamia Manchester United, na anasema ataingia kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba "wakati utakapowadia. (De Telegraaf)
Tottenham wanamfuatilia winga wa Watford Adrian Blake, 17, ambaye mkataba wake yake inamalizika msimu wa joto. (Mail)
Borussia Monchengladbach hawataki kumpoteza kiungo wao Manu Kone katika dirisha lijalo la majira ya jotot huku Chelsea wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21. (Caught Offside)
Wachezaji zamani wa Ufaransa na Arsenal Patrick Vieira na Thierry Henry huenda wakapigania nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanaume ya Marekani. (Goal)
Paris St-Germain wako tayari kutoa kiasi cha euro milion 180 (Β£159m) ili kupata saini ya winga wa Napoli na Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 22. (Corriere dello Sport)
Kipa wa Senegal Edouard Mendy, 31, ameambiwa anaweza kuondoka Chelsea msimu huu wa joto. (Mirror) Bosi wa zamani wa England Roy Hodgson, 75, yuko tayari kurejea tena katika klabu ya Crystal Palace kwa mkataba wa mpaka mwisho wa msimu huu baada ya mazungumzo mazuri mwishoni mwa juma.(Sun)
Chelsea wanafikiria kujenga uwanja mpya Stamford Bridge ambao unaweza kugharimu hadi £2bn na utawahusisha kucheza kwenye uwanja mwingine kwa miaka minne, viwanja wanavyoweza tumia kwa muda ni Craven Cottage, Twickenham na Wembley (Mail)
BBC