Xavi amshawishi Messi arudi Barcelona

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st March 2023


Xavi amshawishi Messi arudi Barcelona

Kuna uwezekano mkubwa Lionel Messi akajiunga na Fc Barcelona mwishoni mwa msimu pale mkataba wake na PSG utakapomalizika

Licha ya sasa kuhusishwa na timu mbalimbali za Uarabuni na Marekani, ila taarifa za ndani kutoka Hispania na Argentina zinadai staa huyo wa klab ya PSG huenda akarejea tena Barcelona

Messi amekuwa na mawasiliano ya karibu na kocha wa Barcelona Xavi Hernandez, ambaye walicheza nae katika kikosi cha Barca kilichoshinda mataji mengi zaidi

Bado mpaka sasa Lionel Messi hajathibitisha kuwa ataendelea kusalia PSG ama atatimkia Uarabuni ama atarejea ndani ya klab ya Barcelona


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.