Azam - Al Hilal

Ibenge ahusishwa na Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Mar 2023
Ibenge ahusishwa na Azam Fc

Wakati Azam FC ikibakiza mechi tano kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara, tayari imeanza kimyakimya kutafuta kocha mpya atakayeiongoza msimu ujao ambao imepania kutwaa ubingwa huku kocha wa Al Hilal ya Sudan, Mkongomani Florent Ibenge akitajwa

Azam ilianza msimu huu ikiwa na kocha Mmarekani mwenye asili ya Somalia Abdihamid Moalin, ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa ikafanya usajili mkubwa, lakini baadaye akaondoshwa kutokana na mwenendo mbaya na mikoba yake kuchukuliwa na Mfaransa Denis Lavagne.

Hata hivyo Lavagne alifukuzwa na timu kubaki chini ya kocha wa makipa Mhispania Dani Cadena akisaidiwa na Kally Ongala na kocha mchezaji Aggrey Morris ambao uongozi upo kwenye mchakato wa kuwaletea bosi wao.

aarifa kutoka ndani ya Azam zinaeleza, mabosi wana majina ya makocha wanne mezani akiwemo Ibenge ambao wanajadiliwa ili apatikane mmoja atakayetua Chamazi kabla ya msimu huu kumalizika ili akione kikosi kilichopo, apendekeze usajili na aende na timu kujiandaa na msimu kuhakikisha lengo la ubingwa linatimia.

Chanzo kimeeleza, katika majina hayo hakuna kocha mzawa hata mmoja lakini moja ya majina ambayo matajiri hao wa Chamazi wanawaza kumwaga pesa kulipata ni Ibenge anayekinoa kikosi cha Al Hilal ya Sudan.

Inaelezwa mabosi wa juu wa Azam wanaamini wakimpata Ibenge ataibadili timu ndani ya muda mfupi kama alivyofanya Al Hilal na kufikia malengo na tayari wamemtumia ofa ambayo bado hajaijibu licha ya kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara baina ya pande zote mbili.

Azam kwa sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo na alama 47 nyuma ya vinara Yanga wenye 65, Simba (57) na Singida Big Stars (48).

Mwanaspoti

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’