Yanga

Yanga yaanza mawindo ya TP Mazembe

Joel JJ By Joel JJ
23 Mar 2023
Yanga yaanza mawindo ya TP Mazembe

Baada ya mapumziko ya siku tatu, kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini leo kuanza maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe. Mchezo huo utapigwa April 02 huko Lubumbashi katika uwanja wa TP Mazembe

Utakuwa mchezo wa kukamilisha ratiba Yanga ikiwa tayari imefuzu robo fainali ya michuano hiyo lakini Wananchi wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza wakiwa vinara wa kundi

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji watashiriki mazoezi na kurejea makwao lakini March 27 wataingia kambini Avic Town kwa ajili ya kukamilisha maandalizi kabla ya safari ya DR Congo itakayokuwa March 30

Nyota wote ambao hawana majukumu ya timu za Taifa, wanashiriki program hizo za mazoezi. Wachezaji 12 wako katika majukumu ya timu za Taifa

Wachezaji walio kwenye majukumu ya timu za Taifa ni walinda lango Djigui Diarra (Mali), Metacha Mnata (Tanzania)

Mabeki Kibwana Shomari, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Bakari Nondo Mwamnyeto (Tanzania)

Viungo ni Mudathir Yahya, Feisal Salum (Tanzania), Khalid Aucho (Uganda), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso)

Washambuliaji ni Fiston Mayele (DR Congo) na Kennedy Musonda (Zambia)

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
22m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →