Misri

VAR ya simu yamponza mwamuzi Misri

Joel JJ By Joel JJ
24 Mar 2023
VAR ya simu yamponza mwamuzi Misri

Mwamuzi wa Misri Mohamed Farouk amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana baada ya kutumia simu ya mtazamaji kukataa bao katika mechi ya ligi daraja la pili

Al-Nasr walidhani walikuwa wamefunga bao la kusawazisha dakika za lala salama wakiwa ugenini kwa Suez katika mechi ya ligi ya daraja la pili

Hakuna mwamuzi msaidizi wa video (VAR) katika daraja la pili la Misri, lakini Farouk alitumia simu kutazama video ya marudio baada ya wenyeji kulalamika kuwa kuna mchezaji aliyeugusa mpira kwa mkono

Farouk kisha alifanya uamuzi wa kulikataa bao hilo. Shirikisho la Soka la Misri lilisema katika taarifa yake kwamba Vitor Pereira, ambaye alichukua nafasi ya Mark Clattenburg kama mkuu wa Kamati ya Waamuzi wa Misri mapema mwezi huu, aliamua kuwasimamisha kazi waamuzi wote kwa muda usiojulikana

"Kamati iliamua kuchunguza tukio wakati Mohamed Farouk, mwamuzi wa mechi hiyo alipotumia simu ya mkononi kukagua picha za matukio ya mechi hiyo," FA ya Misri iliongeza.

Suez ilifunga bao la tatu muda mfupi baada ya bao lililokataliwa na kupelekea ushindi wa 3-1, zikiwa zimesalia dakika 15 kwenda mapumziko

Farouk aliondoka uwanjani chini ya ulinzi wa polisi, huku kukiwa na maandamano ya wachezaji na viongozi wa Al-Nasr, ambao wametishia kumchukulia hatua za kisheria mwamuzi huyo kwa kukiuka kanuni

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
3h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
3h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
3h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
5h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →