Jana Cristiano Ronaldo aliweka rekodi ya Kimataifa ya mechi 197 kwa wanaume kwa kufunga mara mbili Ureno ilipoichapa Liechtenstein 4-0 katika mchezo wa kwanza wa kufuzu Euro 2024.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 sasa amefunga mabao 120 ya kimataifa kwa rekodi ya wanaume.
Alianza mechi yake ya kimataifa mwaka 2003 na nchini Qatar mwaka jana akawa mchezaji wa kwanza kufunga katika michuano mitano ya Kombe la Dunia.
Ronaldo aliongeza idadi ya mabao yake kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili kabla ya kufunga tena kupitia mpira wa adhabu
Ronaldo alikuwa amelingana na fowadi wa Kuwait, Bader Al-Mutawa katika mechi 196 kwenye Kombe la Dunia lakini kulikuwa na maswali kuhusu mustakabali wake wa kimataifa baada ya Ureno kutolewa na Morocco katika hatua ya robo fainali.
Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or alijikuta akiondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha Ureno kwenye michuano hiyo lakini akaridhia kuchaguliwa kwake kuwa nahodha katika mchezo wa kwanza wa meneja mpya Roberto Martinez