Jina la Kocha Mkuu wa Real Madrid, Carlo Ancelotti limeonekana kuwa kivutio kikubwa nchini Brazil
Ancelotti anakipigiwa chapuo arithi mikoba ya Adenor Leonardo Bacci maarufu Tite aliyejiuzulu baada ya michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika Qatar
Rais wa Chama cha Soka Brazil (CBF) Ednaldo Rodriguez amesema Ancelotti anaweza kuwa chaguo sahihi kwa Brazil
Ednaldo amesema Ancelloti anapendwa na mashabiki na hata wachezaji wa Brazil aliowahi kuwafundisha wamempendekeza
"Popote ninapoenda ndani ya Brazil, Ancelotti ndilo jina la kwanza ambalo mashabiki huulizia. Tusubiri muda muafaka tutaona kama tunaweza kuifanikisha" alisema Ednaldo



