Simba kuifuata Raja Casablanca leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th March 2023


Simba kuifuata Raja Casablanca leo

Msafara wa kikosi cha Simba unaondoka jijini Dar es salaam leo saa tisa Alasiri kuelekea Morocco kukamilisha hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca

Taarifa iliyotolewa na Simba, imebainisha kuwa msafara huo utapitia Doha, Qatar na watawasili Morocco siku ya Jumatano asubuhi

Msafara utajumuisha wachezaji 13 huku nyota wengine ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa wataungana na timu huko Morocco

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji saba hawatasafiri kutokana na sababu mbalimbali

Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' ana kadi mbili za njano wakati Jonas Mkude, Mohammed Mussa, Jimmyson Mwanuke na Ismail Sawadogo ni majeruhi huku Mohammed Ouattara akibaki kwa kukosa 'fitness'

Simba itachuana na Raja usiku wa kuamkia Jumamosi, April 01, saa 7 usiku


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.