Klabu ya Tottenham Hotspurs imeanza mazungumzo na kumuajiri aliyekuwa Kocha wa Bayern Munich Julian Nagelsmann, vyombo vya habari Uingereza vimeripoti
Nagelsmanm alitimuliwa na Bayern Munich Ijumaa iliyopita nafasi yake ikichukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel
Hata hivyo imeelezwa kuwa Nagelsmann atahitaji muda kidogo wa kupumzika kabla ya kurejea kwenye majukumu ya soka
Daniel Levy, Mwenyekiti wa Spurs anavutiwa sana na kocha huyo ambaye hata kama watafikia nae makubaliano huenda akajiunga na Spurs baada ya msimu huu kufikia tamati.
Nagelsmann pia anaonekana kuvutiwa na Spurs ambapo mwaka 2019 alinukuliwa akisema kuwa anapenda sana kuangalia mechi ya klabu hiyo
Spurs wamekuwa katika harakati za kutafuta kocha baada ya kumrimua Antonio Conte