Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Raja Casablanca ambao utapigwa usiku wa kuamkia Jumamosi
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kulekea mchezo huo, Robertinho amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo ambao malengo yake ni kusaka ushindi
"Tumekuja hapa kushindana, tumefanya maandalizi mazuri tukiwa na malengo ya kucheza vizuri na kupata ushindi," alisema Robertinho
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wa Simba, kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza amesema pamoja na changamoto ya uchovu unaowakabili, wamejiandaa vyema na watapambana ili kupata matokeo mazuri katika mchezo huo
"Tumekuwa na maandalizi mazuri, japo tuna uchovu wa safari, hiyo haiwezi kuwa sababu kwani wachezaji tunajua wajibu wetu tutapambana ili tupate matokeo mazuri," alisema
Simba iliwasili Morocco majira ya mchana ambapo baada ya mapumziko ya saa kadhaa Simba itafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mohammed V saa nne usiku kwa saa za Morocco ambapo Tanzania itakuwa saa saba usiku