Mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood hatarejea kunako klabu hiyo hadi msimu ujao, imeripotiwa. Greenwood(21) amesimamishwa na klabu yake tangu Januari 2022 aliposhtakiwa kwa mara ya kwanza kwa jaribio la kubaka na kushambulia
Alikamatwa na kufunguliwa mashtaka, hata hivyo, mashtaka hayo yalitupiliwa mbali na polisi
Mustakabali wa Greenwood bado haufahamiki huku Man United wakifanya uchunguzi wa ndani.
Gazeti la Daily Mail linaripoti kwamba hii 'haitakamilika kabla ya majira ya joto’' ikimaanisha kuwa Greenwood hatarejea msimu huu
Ripoti hiyo inasema kuwa Man United ilikataa kuzungumzia lolote. Ripoti hiyo inaongeza kuwa klabu hiyo 'haitaharakishwa kufanya uamuzi' na wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mazingira ya kukamatwa kwake na mwenendo wake nje ya uwanja.
Matatizo ya kimaadili, kiutu, kifedha na kibiashara yanaizunguka kesi ya Greenwood huku wachezaji wa timu ya wanaume na wanawake ya Man United wakiripotiwa kuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa yeye kurejea.
The Mail pia inasema kwamba kuna mgawanyiko katika klabu na 'wafanyikazi wakibishana kuwa anastahili nafasi ya pili, lakini watendaji wa kibiashara wanahofia juu ya uharibifu brand unaoweza kutokea