Jana Yanga ilifanya mazoezi ya kwanza ndani ya Lubumbashi kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa kesho Jumapili, saa 10 jioni
Yanga imepewa nafasi ya kutumia uwanja wa TP Mazembe kufanya mazoezi kwa siku mbili ambapo leo majira ya saa 9 Alasiri (saa 10 Tanzania) watakamilisha mazoezi ya mwisho
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema ari ya wachezaji iko juu kuelekea mchezo huo ambao wanahitaji kushinda ili kujihakikishia kumaliza kileleni mwa kundi D
Harrison amesema wachezaji Fiston Mayele na Stephane Aziz Ki wataungana na wenzao leo wakicheleweshwa na majukumu ya timu za Taifa








