Simba - Local

Kapombe, Kibu hatihati kuikosa Ihefu Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Apr 2023
Kapombe, Kibu hatihati kuikosa Ihefu Fc

Klabu ya Simba imethibitisha wachezaji wake wawili Shomari Kapombe na Kibu Denis walipata majeraha kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Raja Casablanca ambao ulipigwa nchini Morocco usiku wa kuamkia Jumamosi na Raja kuibuka na ushindi wa mabao 3-1

Taarifa iliyotolewa na Simba jana, ilibainisha kuwa wachezaji hao watafanyiwa uchunguzi wa majeraha waliyopata ili kuanza program za matibabu

Kapombe na Kibu wanaungana na winga Peter Banda ambaye pia atafanyiwa uchunguzi wa majeraha ya bega aliyopata wakati akiitumikia timu ya Taifa ya Malawi

Huenda nyota hao wakakosa mchezo wa robo fainali kombe la FA ambao Simba watacheza na Ihefu Fc April 07 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

Simba inatarajiwa kurejea mazoezini siku ya Jumanne baada ya muda wa siku mbili za mapumziko ambao wachezaji wa timu hiyo walipewa baada ya kurejea kutoka Morocco

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’