Azam Fc yatinga nusu fainali kombe la FA

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd April 2023


Azam Fc yatinga nusu fainali kombe la FA

Azam Fc imekuwa klabu ya pili kutinga nusu fainali kombe la FA baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa robo fainali uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Licha ya kucheza pungufu kwa takribani dakika 60 baada ya Daniel Amoah kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi CHarles Ilanfya, Azam Fc bado ilikuwa bora mbele ya Mtibwa Sugar

Mabao ya Azam yalifungwa katika kila kipindi kuputia kwa Kipre Junior na Abdul Suleiman Sopu

Azam Fc imeungana na Singida BS kuwa timu za kwanza kutinga nusu fainali kombe la FA

Mshindi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Ihefu Fc atachuana na Azam Fc katika nusu fainali wakati mshindi wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Geita Gold atachuana na Singida BS


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.