Meneja wa muda wa Chelsea Bruno Saltor amesema wachezaji wa klabu hiyo wako kwenye huzuni kufuatia taarifa za kufutwa kazi kwa kocha mkuu Graham Potter
Saltor (42) raia wa Uhispania kwa sasa anakiandaa kikosi hicho kuelekea mchezo wa Ligi kuu England dhidi ya Majogoo, Liverpool siku ya leo Jumanne.
Chelsea ilimfuta kazi Graham Potter kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya Aston Villa na kumfanya Meneja huyo raia wa England kuwa kocha wa 13 kufungishwa virago mpaka sasa msimu huu.
Mkufunzi Julian Nagelsmann ambaye naye alioneshwa mlango wa kutokea wiki iliyopita huko Bayern Munich anahusishwa na kuchukua mikoba ya Potter huko darajani.



