Aleksandar Mitrovic amefungiwa mechi nane baada ya kumsukuma mwamuzi Chris Kavanagh katika mechi ya Fulham ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United mnamo Machi 19.
Mitrovic alikuwa tayari kukabiliwa na adhabu ya kutocheza mechi tatu baada ya kupokea kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa unyanyasaji baada ya kumwekea mikono Kavanagh, ambaye alikuwa ametoka kuwatoa nje fowadi wa Fulham Willian na kocha mkuu Marco Silva
Mshambulizi huyo wa Serbia alitumikia mechi ya kwanza ya kufungiwa kwake katika mechi ya Jumamosi waliyochapwa 2-1 na Bournemouth kwenye Ligi ya Premia