Benzema apiga hat-trik Real Madrid ikiinyoa Barcelona 4-0

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th April 2023


Benzema apiga hat-trik Real Madrid ikiinyoa Barcelona 4-0

Real Madrid imetinga fainali ya Copa del Rey kibabe katika uwanja wa Camp Nou baada ya kuifumua Barcelona mabao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali

Mshambuliaji Karim Benzema aliendeleza moto wake wa kuzifumania nyavu akiweka hat-trik akifunga mabao hayo baada ya Vinicius Junior kuitanguliza Real Madrid

Barcelona wameondoshwa katika michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 4-1 wao wakipata ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Santiago Bernebeu

Baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo dhidi ya Barcelona, ni kama Real Madrid wamelipa kisasi cha machungu yote waliyopitia

Mashabiki wa Barcelona walikuwa wakiimba jina la Lionel Messi wakati wa wakifedheheshwa. Nyota huyo wa Paris Saint-Germain atashuhudia mkataba wake nchini Ufaransa ukimalizika mwishoni mwa msimu huu na inazidi kuwa wazi kuwa huenda asiongezee tena

Benzema alizima keleke za mashabiki wa Barca kwa hat-trick ya aina yake na kufanya mchezo huo kuwa kipigo cha mabao 4-0 na kuwaondoa kwenye michuano ya Copa del Rey

Mabao yake matatu pia yalimfanya kuwa mfungaji bora wa tatu wa El Clasico kwa Los Blancos, nyuma ya Cristiano Ronaldo na Alfredo Di Stefano


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.