Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anakabiliwa na mchezo mwingine mgumu ligi kuu ya Premia dhidi ya Arsenal siku ya Jumapili katika dimba la nyumbani, Anfield
Liverpool wametoka kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Chelsea katika mchezo uliopigwa Stamford Bridge Jumatano usiku
Klopp hakuwafurahisha mashabiki wa Liverpool katika mchezo dhidi ya Chelsea baada ya kuwaacha nje Mo Salah, Alexander-Arnold na Andy Robertson lakini alieleza kufurahishwa na jinsi timu yake ilivyocheza
Liverpool wanakwenda kuchuana na Arsenal 'wakati mbaya' kwani huenda wakaendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji wao muhimu
Safu ya kiungo imekuwa ikisumbua kwa muda Thiago Alcantara na Naby Keita wakiwa majeruhi, Stefan Bajcetic na Arthur Melo pia hawawezi kucheza Jumapili.
Jordan Henderson na Fabinho wanatazamiwa kushikilia eneo la kiungo. Mo Salah atarejea katika nafasi yake ilhali Klopp ana uamuzi mgumu kufanya safu ya ulinzi upande wa kulia kwa sababu Joe Gomez alicheza vyema dhidi ya Chelsea na Alexander-Arnold hana mwendelezo mzuri msimu huu
Kwa upande wa Arsenla, Mikel Arteta amesema William Saliba hatakuwepo katika mechi hiyo licha ya matumaini yake kuwa beki huyo wa kati atapona mapema jeraha la mgongo
Saliba aliumia kwenye mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Sporting wiki tatu zilizopita. Arteta alidokeza kuwa Rob Holding ataendelea kudhibiti safu ya ulinzi pamoja na Gabriel na kuongeza kuwa anafahamu kabisa kuwa Anfield siku zote ni mahali pagumu kwa The Gunners kushinda.



