Mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Simba na Ihefu utapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi leo Ijumaa, April 07 saa 1:00 usiku badala ya kuchezwa Uwanja wa Uhuru kama ilivyotangazwa hapo awali
Uwanja wa Uhuru una matumizi mengine na kulazimisha waandaaji wa michuano ya ASFC, Shirikisho la Soka (TFF) kuhamishia huko kwa kushauriana na wenyeji wa pambano hilo
Aidha mchezo mwingine wa robo fainali kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa kesho Jumamosi, April 08 nao utapigwa dimba la Azam Complex
Klabu ya Yanga imechagua kutumia uwanja wa Azam complex katika mechi zake za ligi na FA baada ya uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa kupisha ukarabati
