Jahazi la Polisi Tanzania linazidi kuzama baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Singida BS katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Liti, Singida
Mabao ya Paschal Wawa, Nickson Kibabaje na Amis Tambwe yalitosha kuihakikishia Singida BS alama tatu muhimu ambazo zinaendelea kuwaimarisha katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi
Singida BS imefikisha alama 51 ikiwa mbele kwa alama nne dhidi ya washindani wake katika nafasi ya tatu Azam Fc wenye alama 47 kabla ya mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar
Polisi Tanzania wanaendeleza kuburuza mkia katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 19 zikiwa zimesalia mechi nne

