Geita Gold mikononi mwa Yanga robo fainali FA

Joel JJ By Joel JJ β€’ 8th April 2023


Geita Gold mikononi mwa Yanga robo fainali FA

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga leo majira ya saa 2 usiku watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam kumenyana na Geita Gold katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Wakiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Yanga inasaka ushinda ili kukata tiketi ya kutinga nusu fainali

Hata hivyo wanakutana na Geita Gold ambayo mara kadhaa imekuwa sio timu rahisi pale ilipokutana na Yanga

Mara ya mwisho Yanga na Geita Gold zilikutana hapohapo kwenye uwanja wa Azam Complex kwenye mchezo wa ligi kuu Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1

Geita Gold waliweka kambi ya takribani wiki moja jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo huku Afisa wao wa habari Hemed Kivuyo akitamba kuwa leo watalipa kisasi

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo, mlinda lango Aboutwalib Mshery ndiye mchezaji pekee ambaye atakosekana akiwa ni majeruhi

Mshindi wa mchezo huo ataungana na Singida BS, Azam Fc na Simba ambazo tayari zimetangulia nusu fainali


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.