Leo Jumatatu April 10, Ihefu Fc ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Highland Estates, Mbarali huko Mbeya, itachuana na Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Timu hizo zilikutana jijini Dar es salaam juzi kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Ihefu Fc kukubali kichapo cha mabao 5-1
Simba pia ilishinda kwa bao 1-0 mchezo wa duru ya kwanza wa ligi dhidi ya Ihefu Fc uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ikiwa Mbarali, msimu huu Ihefu imejipambanua kuwa timu ngumu kufungika, je wataweza kuendeleza ubabe wao mbele ya Simba inayopigia hesabu ubingwa wa ligi kuu msimu huu?
Simba tayari imetua mkoani Mbeya ikiwa na kikosi chake kamili kikimjumuisha mshambuliaji Jean Baleke aliyefunga hat-trik katika mtanange wa FA
Ihefu Fc ilizifunga Yanga na Azam Fc hapo Real Estate lakini pasipo na shaka watakuwa na kazi kuweza kupata ushindi mbele ya Simba iliyoimarika chini ya Kocha Robertinho Oliveira
Ihefu wametangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni




