Liverpool na Arsenal zimetoshana nguvu katika mechi ya kibabe iliyopigwa uwanja wa Anfield na kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Kikosi cha Mikel Arteta kilianza vyema na kuongoza kwa mabao mawili kupitia kwa Gabriel Martinelli na Gabriel Jesus kabla ya Mohamed Salah kurudisha bao moja kabla ya kipindi cha kwanza.
Tukio la kushangaza likaonekana wakati wa mapumziko pale mwamuzi msaidizi, Constantine Hatzidakis, alionekana kumpiga kiwiko Andrew Robertson
Kipindi cha pili, Liverpool walitawala lakini Salah alikosa penalti kabla ya Roberto Firmino kuingia akitokea benchi na kusawazisha dakika za lala salama.
Liverpool karibu washinde lakini Aaron Ramsdale aliokoa mabao mawili bora na kuwanyima Salah na Ibrahima Konate huku The Gunners wakipata pigo katika mbio za ubingwa
Arsenal sasa wako pointi sita mbele ya Manchester City, wakiwa wamecheza mechi zaidi.