Leicester City - International

Kocha wa zamani Aston Villa atua Leicester

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Apr 2023
Kocha wa zamani Aston Villa atua Leicester

Dean Smith ameteuliwa kuwa kocha wa Leicester City hadi mwisho wa msimu huu

Smith, 52, aliondoka Norwich mapema msimu huu baada ya kuzitumikia Aston Villa na Brentford

Leicester wako katika hatari ya kushuka daraja kufuatia kipigo cha nyumbani dhidi ya Bournemouth Jumamosi iliyopita. Wako pointi mbili kutoka kwa usalama zikiwa zimesalia mechi nane.

"Changamoto iliyo mbele yetu inaeleweka, lakini mimi na timu yangu ya kufundisha tumewahi kuipitia," Smith aliambia tovuti ya klabu.

"Kwa ubora katika kikosi hiki na idadi ya michezo iliyosalia, inawezekana sana"

Mchezo wa kwanza wa Smith kuinoa Leicester utakuwa ugenini dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City Jumamosi.

Craig Shakespeare anarudi King Power Stadium kama meneja msaidizi wa Smith.

Shakespeare alikuwa sehemu ya kikosi cha Claudio Ranieri wakati Leicester iliposhinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza mwaka wa 2016.

Baadaye alichukua nafasi ya Mtaliano huyo kama meneja. Benchi la ufundi la Smith pia litajumuisha nahodha wa zamani wa Uingereza John Terry, ambaye alihudumu chini yake Aston Villa, pamoja na makocha wa sasa wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo Adam Sadler na Mike Stowell.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
40m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’