Manchester United wametikiswa na uwezekano wa kuumia kwa Marcus Rashford huku mbio za kutinga hatua ya nne bora zikizidi kupamba moto.
United wameandikisha ushindi mfululizo dhidi ya Brentford na Everton na kuongeza nafasi zao za kufuzu Ligi ya Mabingwa, lakini inaonekana wamewapoteza Luke Shaw na Rashford kutokana na majeraha
Mshambuliaji huyo amepata jeraha la paja na anatarajiwa kuwa nje kwa wiki kadhaa.
Rashford alipata majeraha hayo katika ushindi wa 2-0 wa United dhidi ya Everton siku ya Jumamosi
Tayari ameondolewa kwenye mechi ya Alhamisi ya robo fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Sevilla na klabu hiyo inatarajia kuwa Rashford atakuwa nje ya uwanja kwa wiki chache
"Tathmini ya jeraha ilipendekeza kuwa Marcus hatapatikana kwa mechi chache, lakini anatarajiwa kurejea kwa msimu katika wiki za mwisho za msimu," ilisema taarifa ya manchester United