Leo Jumatano, April 12 Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana kujadili maombi ya mchezaji Feisal Salum kwa Kamati hiyo akiomba mkataba wake na klabu ya Yanga uvunjwe
Katika kusikilizwa shauri hilo, Feisal aliongozana na wakili wake Fatma Karume ambaye baada ya kumaliza kusikilizwa amesema kuna vitu vya kisheria vinatakiwa kuwasilishwa Aprili 18 na 25 na Mei 4 ndipo rasmi shauri litasikilizwa tena
"Tunasubiri Mei 4 tutasikilizwa," alisema Karume ambaye aliulizwa kuhusu uelekeo wa sakata hilo na kusema hana chochote cha kuzungumza
Nae Mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick amesema madai yoyote ambayo Feisal anayo anapaswa kuyafikisha kwa Mtendaji Mkuu wa Yanga ili yasikilizwe
"Anayemuhitaji Feisal aje klabuni au yeye akitaka kuondoka aje klabuni utaratibu anaujua tupeane mkono wa kwaheri," alisema Simon



