Mane kikaangoni Bayern

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th April 2023


Mane kikaangoni Bayern

Mshambuliaji wa Bayern Munich raia wa Senegal Sadio Mane anatarajiwa kuomba msamaha katika mazoezi ya Bayern Munich hii leo

Ni baada ya kitendo cha kumpiga Leroy Sane baada ya kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Man City siku ya Jumanne kwenye robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya

Viongozi wa Bayern walikutana jana na kujadili tukio hilo ambalo wanaona limeichafua taswira ya klabu hiyo

Mabosi wa Bayern wanazingatia adhabu mbalimbali kwa Mane ikiwa ni pamoja na faini, kusimamishwa kazi au kuondoka katika majira ya joto


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.