Kikosi cha Simba kiliingia kambini jana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumapili, April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kurejea kikosini kwa wachezaji wao waliokuwa majeruhi
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji wote wako tayari kushiriki mchezo huo
"Timu imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga. Wachezaji wote ikiwa pamoja na wale waliokuwa Mbeya kuikabili Ihefu Fc, waliingia kambini na wenzao waliokubwa wamebaki jijini Dar es salaam kutokana na sababu mbalimbali"
"Hata wachezaji ambao walikuwa majeruhi nao wamepona, ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo huo," alisema Ahmed
Miongoni mwa wachezaji waliokuwa majeruhi ni pamoja na mlinda lango Aishi Manula, Hennock Inonga na Shomari Kapombe
Manula na Innonga walipata majeraha kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Ihefu Fc uliopigwa uwanja wa Azam Cmplex na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 5-0
Kapombe aliumia katika mchezo wa kukamilisha ratiba makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca
Kurejea kwao ni habari njema kwa Simba kuelekea mchezo dhidi ya watani zao ambapo Simba inasaka ushindi wa kwanza kwenye ligi tangu washinde kwa mara ya mwisho Februari 2019