Derby imebeba hatma yetu kwenye ubingwa - Mgunda

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th April 2023


Derby imebeba hatma yetu kwenye ubingwa - Mgunda

Kocha Msaidizi wa Simba Juma Mgunda amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumapili April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa yanaendelea vizuri

Mgunda amesema mchezo ulifahamika muda mrefu hivyo kwa sasa hawafanyi maandalizi mapya ila kinachofanyika ni maandalizi ya mwisho ya kiufundi

"Mchezo huu tuliufahamu muda mrefu hivyo sio kwamba tumeanza maandalizi mapya hapana, tayari tulishajiandaa kinachofanyika sasa ni kukamilisha maandalizi tu"

"Tunajua ni mchezo mzito ambao unashikilia hatma yetu katika mbio za ubingwa. Siku zote nasema haiwi mwisho mpaka ifike mwisho. Bado tuko kwenye mbio za ubingwa"

"Bingwa atapatikana  baada ya msimu kumalizika hivyo tunauchukulia mchezo huu kwa umuhimu mkubwa," alisema Mgunda

Kuhusu utayari wa kikosi, Mgunda amesema wachezaji wote wanaendelea vyema na maandalizi, nyota waliokuwa majeruhi wamerejea kikosini pia


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.