Yanga - Local

Tumejiandaa kushinda dhidi ya Simba - Nabi

Joel JJ By Joel JJ
13 Apr 2023
Tumejiandaa kushinda dhidi ya Simba - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi wamejifungia Avic Town kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba abao utapigwa Jumapili, April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kila Mwananchi anafahamu umuhimu wa mchezo huo ambapo matokeo ya ushindi yatakuwa yameihakikishia Yanga ubingwa kwa zaidi ya asilimia 80

Nabi anajivunia ubora wa kikosi chake akiamini maandalizi yao yatatosha kuwafanya wawe na ubora mkubwa kwenye mchezo huo

"Tunawaheshimu Simba ni timu yenye mabadiliko lakini hatuwezi kuwa na presha hata kidogo, tunakwenda kuandaa timu ambayo itakuja uwanjani kucheza kwa ubora mkubwa kwenye mechi hii kubwa, tunawajua vizuri sana," alisema Nabi

Nabi tangu ajiunge na Yanga April 2021, ndani ya mechi 8 za mashindano yote dhidi ya Simba ameshinda 4 akipoteza 1 na kutoa sare 3

"Kitu bora kwetu wachezaji ambao walikuwa majeruhi wamerejea, hii itatupa nafasi pana ya kuchagua nani anaweza kuwa ndani ya kikosi kuelekea mchezo huo"

"Malengo yetu ni kuendelea kushinda, tunahitaji ushindi ili kuendelea kuweka hai malengo ya kuchukua ubingwa wakati kama huu ni vyema kuongeza pointi na sio kupunguza"

"Narudia tunaiheshimu Simba na hautakuwa mchezo rahisi lakini niseme Yanga itaingia uwanjani kucheza kwa ubora mkubwa kwa ujazo wa mchezo mkubwa kama huo ili tupate ushindi, jambo la msingi kwetu ni kushinda," aliongeza Nabi

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
3h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
3h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
3h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
5h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →