Ollie Watkins aliendeleza kiwango chake kizuri kwa kufunga mabao mawili huku Aston Villa wakiimarisha matumaini yao ya Uropa kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle
Ulikuwa ushindi wa tano mtawalia kwa Aston Villa kushinda katika Uwanja wa Villa Park
Watkins alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Newcastle kwani angeweza kuondoka na hat-trik kama bao lake lake la kwanza lisingekataliwa na VAR
Kikosi cha Unai Emery kilitawala hatua za awali na kuchukua uongozi uliostahili wakati Jacob Ramsey alipopiga mpira wa kichwa wa Watkins chini kabisa wavuni.
Aston Villa wamepanda mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa alama sita tu nje ya top four baada ya kufikisha alama 50