Mmiliki wa Chelsea Todd Boehly alionekana akikabiliana na mashabiki wenye hasira katika uwanja wa Stamford Bridge baada ya timu yake kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Brighton.
The Blues walitoa uongozi wa mapema na kulala 2-1 dhidi ya Brighton wakiwa nyumbani kwenye Ligi ya Premia, na hivyo kuandikisha kupoteza kwao kwa mara ya 17 msimu huu

Matokeo hayo yameiacha Chelsea ikiwa nafasi ya 11 kwenye jedwali, licha ya kutumia rekodi ya pauni milioni 600 kwa msimu mmoja tangu Boehly alipochukua klabu hiyo.
Akiwa na huzuni kwenye jukwaa la watu mashuhuri, Boehly alionekana kwenye mazungumzo na mashabiki kutoka kwenye stendi iliyo juu baada ya filimbi ya mwisho
Baadaye, mfanyabiashara huyo alionekana akitembea kwenye uwanja wa Stamford Bridge huku ikidhaniwa kuwa alikuwa akielekea kwenye chumba cha kubadilishia nguo