Kocha Msaidizi wa Simba Juma Mgunda amewapongeza wachezaji wa Simba kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani zao Yanga katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana
Mgunda amesema wachezaji walitekeleza maelekezo waliyopewa kwa usahihi na kama wangekuwa na bahati zaidi walistahili kushinda mchezo huo kwa idadi kubwa ya magoli
"Niwapongeze wachezaji wetu kwa ushindi huu. Tulijua ubora wa Yanga na madhaifu yao hivyo tulifanya maandalizi mazuri sana ya mchezo. Kocha (Robertinho) alituambia mapema tusiwape Yanga nafasi ya kuwa na mpira na tukiwa na mpira tuharakishe mashambulizi"
"Kipindi cha kwanza tulipaswa kufunga sio chini ya mabao manne lakini jambo muhimu tumeweza kushinda na niwapongeze wachezaji kwa kufanikisha ushindi huu," alisema Mgunda
Akizungumza kiwango cha mlinda lango Ally Salim, Mgunda alisema walimuandaa kucheza mechi hiyo kabla ya mchezo dhidi ya Ihefu Fc
"Niwaibie siri, tulimuandaa Salim kucheza leo (jana) kabla ya mchezo dhidi ya Ihefu. Baada ya mchezo ule tulimuambia atakuwa na jukumu kubwa la kukaa langoni kwenye mchezo huu"
"Nampongeza amefanya vizuri muhimu aendelee kujituma, umri wake bado mdogo ana nafasi ya kufika mbali zaidi"