Kocha Mkuu wa KMC,Jamhuri Khiwelu, amesema kuwa ana matumaini makubwa ya kuongeza ari kwenye mechi ambazo zimebaki
Julio amechukua mikoba ya Hitimana Thiery ambaye alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo kutokana na mwendo mbovu
Mchezo wa mwisho kwa Hitimana kukaa benchi alishuhudia akipigwa mabao 2-1 na Geita Gold kwenye uwanja wa Uhuru
"KMC ni timu nzuri na nilikuwa ninaifuatilia kwenye mechi zake ambazo ilikuwa inacheza, nina amini kwamba itafanya vizuri kwenye mechi ambazo zimebaki"
"Tutapambana kupata matokeo mazuri ili kuhakikisha tunaendelea kubaki Ligi Kuu. Nafahamu KMC ni moja ya timu ambazo ziko vizuri kiuchumi najua suala la mishahara hapa sio tatizo "
"Jukumu langu ni kuwahamasisha hawa wachezaji watoe zaidi ya kile walichotoa katika mechi zilizopita, naamini hatuwezi kushuka daraja," alisema Julio
Tayari Julio ameanza mazoezi na timu hiyo inayojiandaa na mchezo dhidi ya Dodoma Jiji