VAR kutumika robo fainali CAF

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th April 2023


VAR kutumika robo fainali CAF

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limethibitisha kutumika kwa teknolojia ya usaidizi wa waamuzi kwa njia ya video (VAR) katika mechi za robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika

Klabu za Tanzania Simba na Yanga zitakuwa kwenye majukumu ya kupeperusha bendera ya nchi mwishoni mwa wiki hii kwenye mechi hizo za robo fainali

Jumamosi April 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 10 jioni Simba itawakabili mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Wydad Athletic, VAR itatumika katika mchezo huu wa mkondo wa kwanza na pia itatumika katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Morocco April 29

Jumapili April 23, Yanga itakuwa ugenini huko Nigeria kuikabili Rivers United katika mchezo wa mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho, VAR pia itatumika

Mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30 ambapo teknolojia ya VAR pia itatumika


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.