Yanga kuifuata Rivers United Alhamisi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 18th April 2023


Yanga kuifuata Rivers United Alhamisi

Kikosi cha Yanga kitaondoka nchini Alhamisi kuelekea Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United

Mchezo huo utapigwa Jumapili, April 23 huko Nigeria katika uwanja wa Godswill Akpabio uliopo mji wa Uyo

Rivers United walitumia uwanja huo kwenye hatua ya makundi na baadae wakaomba kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wao wa Adokiye Amiesimaka huko Port Harcort ila Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limegomea mabadiliko hayo baada ya kufanyia ukaguzi uwanja huo na kubaini bado haukidhi vigezo

Yanga inasaka nafasi ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo, itahitaji ushindi au hata matokeo ya sare ugenini kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es salaam

Mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30 2023


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.