Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amekutana na Wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo walioshiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani Aprili 17, 2023
Gabriel Geay aliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo
Mheshimiwa Rais Mstaafu amempongeza Gabriel Geay kwa ushindi mkubwa na kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania
Pamoja na wanariadha hao, walikuwepo pia wahamasishaji mbalimbali akiwemo 'Bongo Zozo'
Aidha, amewapongeza pia kwa kuhamasisha ushindi huu na kufanikisha kuinua bendera ya Tanzania juu
Rais Kikwete yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Harvard



