Simba yasaka ushindi dhidi ya Wydad leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd April 2023


Simba yasaka ushindi dhidi ya Wydad leo

Siku imewadia! Ni mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Simba dhidi ya Wydad Athletic

Ni katika uwanja wa Benjamin Mkapa mchezo huo utapigwa majira ya saa 10 jioni

Mechi muhimu kwa Simba kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali

Katika miaka mitano iliyopita, Simba imecheza robo fainali mashindano ya CAF mara nne, lakini wakati huu dhamira ya Wanamsimbazi ni kuvuka hatua ya robo fainali

Utakuwa mchezo mgumu dhidi ya timu bora ya Wydady, ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo lakini hakuna lisilowezekana kwenye mpira wa miguu

Ikiwa ni sikukuu ya Eid, ushindi utanogesha shamrashamra za ndugu zetu Waislam ambao wanasherehekea sikukuu hii baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amewataka Wanasimba kununua tiketi kwa wingi ili kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.