Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Nabi alisema wanatambua wanakwenda kukabiliana na timu bora lakini malengo yao ni kupata ushindi
Nabi amesema hawataingia kwenye mchezo huo wakifikiri matokeo ya hatua ya makundi na kuwa lazima wawaheshimu wapinzani wao
"Hatujioni wakubwa kwa kuwa tumetoka kuongoza kundi. Tunawaheshimu wapinzani wetu kwani tunatambua ni timu nzuri lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunasonga mbele," alisema Nabi
Mchezo utapigwa kesho Jumapili saa 10 jioni (saa 8 Nigeria) katika uwanja wa Godswill Akpabio International