Jahazi la Ruvu Shooting linazidi kuzama baada ya leo kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro
Ruvu Shooting wako mkiani mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 20 zikisalia mechi tatu tu
Ushindi huo umeipandisha Azam Fc katika nafasi ya tatu ikifikisha alama 53, alama mbili juu ya Singida BS ikiwa na alama 51
